Pishi La Leo Na CHef Beka

Pishi La Leo Na CHef Beka Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Pishi La Leo Na CHef Beka, Kitchen/Cooking, Morogoro.

MAPISHI YA CHAPATI ZA NYAMA .Vipimo Unga                                                            1 ½ vikombe vya chai...
03/05/2025

MAPISHI YA CHAPATI ZA NYAMA .

Vipimo

Unga 1 ½ vikombe vya chai

Mafuta ¼ kikombe cha chai

Chumvi ½ kijiko cha chai

Maji 1 kikombe cha chai

Mafuta ½ kikombe cha chai


Mayai 6 mayai

Manda nyembamba za mraba
(Spring roll pastries sheet) 6


Nyama ya kusaga ½ kilo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi 1 kijiko cha supu

Kotmiri iliyokatwakatwa ½ kikombe

Chumvi kiasi

Pilipili manga ½ kijiko cha chai

Pilipili mbichi kiasi (ukipenda)

Bizari ya pilau ya unga ½ kijiko cha chai.


Namna Ya Kutayarisha Na Kupika



Changanya unga na mafuta ¼ kikombe maji na chumvi pamoja kanda mpaka ulainike

Kata madonge sita, mimina mafuta ½ kikombe kwenye chombo kipana kisha yaroweke madonge kwa muda wa ½ saa hadi saa 1.

Changanya nyama na vitu vyote na ichemshe mpaka iwe kavu k**a nyama ya sambusa , wacha ipoe.

Sukuma donge ulitandaze liwe jepesi, kisha weka juu yake hiyo manda nyembamba ya mraba .

Kwenye bakuli ndogo piga yai moja na vijiko 2 vya hiyo nyama kavu kisha mimina juu ya hiyo manda ya mraba kisha ifunike k**a inavyoonyeshwa kwenye picha.


Choma k**a unavyochoma chapati ila wakati unageuza kutia mafuta toboa toboa na uma ili yai lipate kuiva vizuri ndani kwa moto wa kiasi.

Weka kwenye sahani tayari kuliwa.

Na juice ya matunda baridii

Kwa mapishi zaidi jiunge group whatsapp https://chat.whats

Address

Morogoro

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Pishi La Leo Na CHef Beka posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share